Swali linalojitokeza kwenye ufahamu wa watu wengi, wanaoambiwa kauli iliyotangulia hapo juu, ni hili: nawezaje kuwauzia watu waliopo mtandaoni—hasa hasa kupitia WhatsApp?
Nafahamu kuna wengine miongoni mwetu, tunafahamu namna ya kufanya hivyo, ndiyo maana kuna vikundi vingi vya WhatsApp, vya watu wanaouza bidhaa mbalimbali. Bidhaa kama nguo, viatu, magari, viwanja, vyombo vya majumbani, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi na nyingine nyingi.
Tunahitaji kuendelea kufahamu mambo mapya, na kubadilishana mawazo juu ya namna nyingine mpya inayoweza kutusaidia kuliteka soko kwa urahisi—kupitia WhatsApp.
Tunaweza kukumbushana kuwa: katika suala la kuuzia mtandaoni, kuna bidhaa za aina mbili:
1. Bidhaa halisi zinazoshikika (Physical/Tangible Products).
2. Bidhaa za kidigitali (Digital/ Downloadable Products).
• Katika aina ya kwanza, ndipo kuna vitu kama nguo, viatu, magari, vipodozi, vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme majumbani, simu, na nyingine nyingi.
• Katika aina ya pili, ndipo kuna bidhaa zinazouzwa moja kwa moja mtandaoni—bila kusafirishwa. Mteja anaipata kwa njia ya mtandao. Kwa kutumiwa kwa e-mail au kwa njia nyingine au hata kwa kuipakua (download) kwenye tovuti (website) fulani—baada ya kukamilisha malipo.
Mifano baadhi ya bidhaa zinazohusika hapa ni: vitabu (softcopy—PDF), video, audio, picha, Apps na softwares nyingine. Vilevile kuna huduma ambazo zinatolewa mtandaoni, bila mteja kukutana ana kwa ana na mtoa huduma. Huduma hizo ni kama ubunifu wa graphics (graphic design) na Website Designing and Hosting. Hizo ni baadhi.
Katika aina hii, kila kitu; yaani malipo na makabidhiano ya bidhaa, vinakamilika moja kwa moja mtandaoni.
Katika suala la kutafuta wateja, hivi sasa tunaweza kuwa na watu wengi sana wa kuwafikia—kupitia WhatsApp. Wateja wa aina zote mbili za bidhaa wapo WhatsApp.
Jambo muhimu la kufahamu na kulifanya ni namna nzuri (mpya) ya kuwafikia wengi miongoni mwao, na jinsi ya kuwatambua—kwa ajili ya kuwatangazia bidhaa au huduma yako.
Kitabu chetu cha 'WATEJA WAKO SIO HAO TU' , kina njia nzuri ambazo hivi sasa zinatumika kuhifadhi (save) namba nyingi za WhatsApp, kwa muda mfupi na jinsi ya kuzitumia namba hizo katika:
1. Kuwafikia watu wengi waliopo WhatsApp pasipo kutegemea uwepo wa vikundi vya whatsapp na status pekee. Ili kuwafikia kwa mguso wa karibu, kwa kutumia mbinu ya P2P Sales Prospecting.2. Kuweka na kupima mkakati rahisi wa kuandaa wateja tarajiwa wasio na kikomo kupitia WhatsApp.
KUMBUKA: WhatsApp inakadiriwa kuwa na watumiaji wengi sana.
Dunia nzima: zaidi ya bilioni 2.
Afrika: zaidi ya milioni 525.
Tanzania: zaidi ya milioni 10.
Wengi miongoni mwao, wapo kwenye vikundi mbalimbali vya whatsapp; mahali tunapoweza kupata mawasiliano yao.
FOMATI YA KITABU: PDF (softcopy).
BEI YA KITABU: TSH 2,000/-
NJIA YA KUKIPOKEA: WhatsApp & Baruapepe (e-mail).
MAWASILIANO: 0743 517 138 (WhatsApp).
0763 258 095—malipo (EMMANUEL KIMANISHA).
______________________
UBAO WA MATANGAZO YA MAENEO MENGINE:
---------------------------------
No comments:
Post a Comment